4:58 AM
0
Jumapili hii kwenye kanisa la Ufufuo na Uzima kulikuwa na ibada ya kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kununua chombo cha anga, helikopta ambayo watakwa wanaitumia kwenye kuhubiri injili.
Kutoka makanisani wiki hii inakuletea matukio ya siku hiyo, ambayo yaliambatana na uimbaji uliotukuka kutoka kwa wainjilisti mbalimbali kama vile Upendo Nkone, Christina Shusho, Faustin Munishi (Malebo), John Lisu, Rose Muhando, Florah Mbasha, David Robert, Boniphace Mwaitege, na wengineo wengi.

Ibada hiyo ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya watu, ilkuwa baraka kwa kila mtu kutokana na huduma ya waimbaji, pamoja na mahubiri ambayo Askofu Jospehat Gwajima alihudumu, kuhusu nyota iliyoibiwa. Lakini pamoja na uimbaji uliotukuza jina la Mungu, John Lisu  baada ya kugusa watu na kuzama katika Roho, ndipo hapo Askofu Gwajima akatangaza nia ya kumzawadia gari John Lisu, huku akimuita Don Moen wa Tanzania. Ahadi hiyo inatarajiwa kutimizwa baada ya wiki tatu.

"Kama tumeweza kununua helikopta, itatushinda gari ya John Lisu?" ananukuliwa akisema Askofu Gwajima.

Ambatana nasi kwa matukio haya kuanzia maandalizi yalivyokuwa.

Masaa machache kabla ya tukio (jana yake)
Baadhi ya wanahabari kanisani hapo
Tukio lenyewe
 Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima James Mdee


Baadhi ya waimbaji walikuwepo siku hiyo
Flora Mbasha na timu yake
Upendo Nkone akipoea kipaza
Kwa Yesu kuna amani
Christina Shusho na Mwanamapinduzi madhabahuni
Wachungaji kutoka Japan
 Team John Lisu

0 comments:

Post a Comment