Pande zote mbili katika mazungumzo ya kusitisha vita katika eneo la Gaza zimeonya kuwa mpango wa mazungumzo hayo upo hatarini.
Israel imesema kuwa mazungumzo hayo
yanayotarajiwa kuanza hii leo huko Misri yataendelea tu iwapo wapiganaji
wa Hamas watasita kurusha makombora ya roketi nchini Israel.Hamas nayo imesisitiza kuwa itashiriki katika mazungumzo yasiyo moja kwa moja iwapo Israel itakoma kuweka vikwazo.
Makubaliano ya kusitisha vita kwa saa 72 katika eneo la Gaza yalikamilika siku ya ijumaa.
Tangu siku hiyo,Palestina imesema kuwa watu saba zaidi wameuawa.
Marekani,Uingereza ,Ufaransa na Ujerumani zimetaka makubaliano hayo kuanza kutekelezwa mara moja.
0 comments:
Post a Comment